Capacitar Tanzania hukuza uponaji wa athari za majanga na uwezeshaji kwa njia ya Elimu ya Afya kwa wote. Lengo ni kuwawezesha na kuwaweka huru watu wanaokandamizwa na changamoto mbalimbali za maisha zikiwemo za kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiafya pamoja na kuondoa maumivu ya mwili na msongo unaosababishwa na magonjwa na matatizo mengine ya maisha ili luleta uponaji, amani na umoja katika dunia yetu.
Capacitar International imekuwa msaada mkubwa sana wa uponaji kwa watu wengi. Mpaka sasa inatumia katika nchi zaidi ya 36, Tanzania ikiwemo.
Kila mtu anaweza kufaidika na mazoezi ya Capacitar katika maisha yake ya kila siku. Kwa sasa makundi yafuatayo yanafaidika:

- Vikundi vya vijijini
- Watu wenye UKIMWI na wahudumu wao
- Vikundi vya kijamii
- Walimu na wanafunzi
- Watoto yatima
- Wahanga wa ukatili majumbani
- Vikundi vya dini
- Watoto wanaoishi katika mazingira magumu na walezi wao
- Wagonjwa, wauguzi, na waganga
- Vikundi vya wafanyakazi
- Askari magereza na wafungwa